Sisi ni wataalamu inapokuja kwa lugha

Kwa ufupi, wafasiri wetu wamefuzu vizuri sana. Huwa tunahakikisha jambo hili kabla ya kuanza kufanya kazi na mfasiri, kwa sababu ufasiri wa maandishi ya kiafya yaliyo ya kiufundi, mawasiliano ya kutumia simu na Teknolojia ya Habari huwa unahitaji ujuzi usuli wa utaalam.  Wafasiri wanaojanibisha programu za kompyuta lazima wawe wanaweza kutofautisha kati ya maandishi yanayofaa kutafsiriwa na misimbo ya kuandika programu. Wafasiri wanaofanyia kazi aina zingine za maandishi, kama vile utangazaji au uhusiano, wanafaa wazingatie muundo na malengo ya mwandishi ya uuzaji .
Huduma zetu za fasiri

Kupanga

Kila ufasiri huanza na mazungumzo kati yetu na wewe. Mtu mnayewasiliana na yeye  atakueleza wazi mahitaji yako ya ufasiri na atakushauri njia nzuri ya kufanikisha lengo lako.

Kutumia ufasiri tena

Huwa tunafasiri maandhishi mapya au yaliyorekebishwa. Maandhishi ambayo tayari yashatafisiriwa huhifadhiwa katika kumbukumbu yetu ya ufasiri, ambayo tunaweza kuitumia wakati wote tunapofasiri masasisho. Wafasiri wote wanatumia na kusasisha hifadhidata moja wakati mmoja. Hii inamaanisha kwamba tunaweza kudhamini kiwango cha juu cha udhibiti kwa kila ya kazi yako.

Usimamizi wa kazi ya lunga nyingi

Msimamizi wa kazi yako ndiye anapanga mchakato wote. Yeye ndiye anaratibu rasilimali na tarehe ya mwisho unaohitajika kwa mchanganyiko wa lugha zako, anatayarisha nyenzo za ufasiri na anajibu maswali yoyote ambayo timu ya ufasiri inaweza kuwa nayo. Kazi yetu huwa haiishi mpaka uridhishwe na matokeo.

Ujanibishaji

Wakati ujanibishaji wa programu za kompyuta umefanywa vizuri, kiolesura cha mtumiaji huwa kinafanya kazi kama kilikuwa kimeundiwa soko linalokusudiwa. Kwa kuongezea ufasiri wa maandishi, huwa tunazingatia ukamilifu wa utamaduni na kiufundi wa soko linalokusudiwa, kama vile vizio vya upimaji, umbizo za namba na anwani, na pia sheria na vipimo kamili.

Ufasiri

Kwa usaidizi wa mtandao wetu ulimwenguni wa wafasiri wa kiufundi wanaofanya kazi kwa lugha zao za kuzaliwa, tunaweza kufasiri maandishi yako kwa lugha zote kuu duniani. Tunatoa ufasiri katika nyanja za madawa, mawasiliani ya simu na bidhaa za elektroniki. Nyanja yetu ya kitaalam ni ujanibishaji wa programu za kompyuta.

Hua tunakagua kila ufasiri kuhakikisha lugha na maandishi yako sahihi na yanasomeka. Upitiaji tena wetu unahusu kuangalia utumiaji, ufanyaji na taratibu kwa kusanikisha na kutumia programu iliyojanibishwa. Mchakato huu unatuwezesha kuhakikisha kwamba nyaraka, usaidizi na programu ziko sawa kwa kila lugha inayokusudiwa.

Usimamizi wa istilahi

Istilahi zilizochunguzwa kwa makini ndio msingi wa kila ufasiri wa kiufundi. Tunadumisha istilahi katika kamusi na hifadhidata mahususi kwa kila kazi. Tukitumiwa maombi, tunaweza kuzihalalisha, kuzipanua na kuzisasisha hizo kama sehemu ya mfumo wetu wa usimamizi wa istilahi. Bidii hii yote iko na matokeo mazuri – wafasiri wetu wote wanatumia istilahi za kiufundi zinazolingana kwa kazi zako zote.