Teknolojia inayofaa ni muhimu

Bila ya kusema tuko na maneno ya kiufundi yanayohitajika na uelewaji mkali wa muktadha ya kiufundi. Kufuzu huko kunatumika kama msingi wetu wa kiufundi wakati tunafasiri nyaraka zako na usaidizi wa matumizi.

Vifaa vyetu vya hali ya juu vya ufasiri na ujanibishaji wa programu za kompyuta vinahakikisha kwamba vipengele vyote vya kazi vinalingana.

Ungependa kujua vile teknolojia hii inaweza kukusaidia? Tuulize tu!

Huduma za kiufundi na zinazohusiana na ufasiri

Kumbukumbu za ufasiri

Tunatumia mfumo wa kumbukumbu za ufasiri ambao unataka tuutumie, kama vile SDL Trandos. Ufanyaji wa hifadhidata ya mfumo inahifadhi maandishi asili yakiwa yanaambatana na ufasiri wake, ambayo inamaanisha tunaweza tukalinganisha maandishi asili mapya na ufasiri uliohifadhiwa katika mfumo mara moja. Mfumo wetu ni wa wavuti na unaendeshwa katika seva, inayoruhusu wafasiri wengi – wa ndani na nje – kufanyia kazi faili kwa wakati mmoja, kutumia ufasiri uliopo na kuongeza ufasiri mpya.

Ujanibishaji wa programu za kompyuta

Kifaa kimoja kinachotimiza viwango vya tasnia ni SDL Passolo, inayotoa ufanyaji wa jaribio lililofungamanishwa na violesura kwa kumbukumbu za ufasiri, kama ya ziada kwa ufanyaji wa ufasiri. Passolo ina aunisha umbizo zote za faili na kuchapuza na kurahisisha michakato ya ujanibishaji wa kiufundi. Tunafurahi kuzingatia ombi lako tunapochagua kifaa cha kutumia.

Kubadilisha ukubwa wa programu

Mara nyingi maandishi yanayotafsiriwa huwa sio ya urefu sawa na maandishi ya chanzo. Tunarekebisha urefu wa vidhibiti kuhakikisha kwamba maandishi kamili yanabaki yakionekana katika programu iliyojanibishwa

Msaada wa mtandaoni wa kujaribu programu na kukusanya

Mara tu kazi ya ufasiri imekamilika huwa tunajaribu programu kuhakikisha kwamba lugha iko sahihi na programu inasomeka – na kwamba inafanya kazi vizuri kabisa. Tunakusanya msaada wa mtandaoni na kujaribu yaliyomo na utendaji. Hata hivyo, msaada husaidia tu kama unaeleza kuhusu programu sawasawa.

Uchapishaji ofisini

Tunafurahi kuwasilisha nyaraka katika umbozi sawa na maandishi asili. Na kwa kawaida tunarekebisha mpangilio kulingana na urefu wa maandishi yanayokusudiwa. Ukituomba, tunaweza pia tukakutolea nyaraka zako katika muundo wa kuchapishwa.

Uchakataji wa michoro na picha za skrini

Tunafasiri maandishi ya michoro na vielelezo na kurekebisha mpangilio kulingana na urefu wa maandishi ya lugha inayokusudiwa. Kama nyaraka ziko na picha za skrini za programu, tunaunda matoleo yaliyojanibishwa kwa kutumia programu inayotumika katika lugha inayokusudiwa.

Utaratibu wa video na sauti

Pia tunafasiri maandishi ya utaratibu wa video na sauti. Bila shaka, kufanya hivi tunazingatia ukamilifu wa neno lililotamkwa. Kama unahitaji mbia wa utengenezaji video au sauti, tutafurahi kutoa usaidizi wetu.